Thursday , 31st Jan , 2019

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), limesema litafanyia kazi mapendekezo ya kubadilishwa mfumo wa usajili barani Afrika ili kuwepo na dirisha la pamoja tofauti na sasa ambapo kila nchini ina muda wake wa usajili.

Kocha wa Azam FC

CAF kupitia kwa makamu wake wa Rais Amaju Pinnick, amedokeza kuwa malalamiko hayo yametolewa na vilabu vingi hivyo wataliangalia suala hilo kama litakuwa na manufaa basi watabadilisha.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Azam FC,  Abdulkarim Amin 'Popat', amesema anaunga mkono kwa asilimia 100, kuwa kipindi cha usajili cha uhamisho wa wachezaji kwa nchi za Afrika kinatakiwa kuendana.

''Utaratibu ukiwa wa dirisha la pamoja kwa nchi zote itatoa fursa kwa timu kuziba mapengo au kuuza wachezaji kwenye klabu nyingine'', amesema Popat.

Tofauti na Ulaya ambako kuna vipindi viwili tu vya usajili yaani Julai na Januari, Afrika bado kila nchini ina kipindi chake cha usajili ukiacha zile nafasi ambazo hutolewa na CAF kwa timu zilizofuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa na kombe la shirikisho Afrika.