Akizungumza na East Africa Radio, Kocha msaidizi ambaye pia ni kocha wa magoli Kipa, Manyika Peter amesema, kikosi hicho kimeingia kambini kikiwa hakina idadi maalumu kwani bado kinaendelea kutoa na kuingiza wachezaji kutokana viwango watakavyovipata katika mechi za majaribio watakazocheza.
Manyika amesema, kikosi hicho kinatarajia kuelekea jijini Mbeya siku ya Ijumaa na kinalelewa kwa misingi maalimu ya kisoka ili kukuwa nayo kwa ajili ya kupata wachezaji bora hapo baadaye.
Manyike amesema, kikosi hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo huo kwa lengo la waalimu kupata fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza wengine watakaoonekana katika kikosi hicho.
U 15 ni mpango wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo vijana hao watakuwa na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakapoanza mwezi Julai, 2016.


