Monday , 5th Feb , 2018

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga kupitia kwa daktari wa timu hiyo Dr. Bavu wamesema wachezaji wao 11 ni majeruhi.

''Wachezaji wetu 11 bado ni majeruhi, ni wazi hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya Njombe Mji'', amesema Dr Bavu.

Dr. Bavu amewataja wachezaji hao kuwa ni mlinda mlango Youthe Rostand na walinzi Juma Abdul, Haji Mwinyi, Abdallah Shaibu na Andrew Vicent.

Wengine ni viungo Pato Ngonyani, Thaaban Kamusoko, Ibrahim Ajib na winga Yohana Nkomola. Washambuliaji ni Hamis Tambwe na Donald Ngoma.

Yanga ikiwa bila ya nyota wake hao imefanikiwa kushinda mechi yake dhidi ya Lipuli FC jumamosi iliyopita na kesho itakuwa dimbani kucheza na Njombe Mji kwenye mchezo wa raundi 17.