Thursday , 25th Aug , 2016

Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameamka na kusema, anakubali kufungwa lakini akasisitiza, walicheza mechi kwenye uwanja mbovu.

Jamhuri Kihwelu

Toto African ndiyo walioichapa Mwadui FC kwa bao 1-0, katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Shujaa wa Toto katika mchezo huo alikuwa ni Waziri Junior aliyepachika bao hilo katika kipindi cha kwanza.

"Tumefungwa sawa. Lakini uwanja tuliochezea, hauna viwango na umeharibika sana".