Tuesday , 31st May , 2016

Mahakama kuu ya Uhispania imeanza kusikiliza kesi juu ya tuhuma za kukwepa kulipa kodi dhidi ya mchezaji nyota duniani Lionel Messi.

Raia huyo wa Argentina na mshambulizi wa Barcelona, anakabiliwa na mashtaka ya udanganyifu na kukwepa kulipa kodi takriban dola milioni 4.5 kati ya mwaka wa 2007 na 2009.

Messi na babake Jorge, ambaye ndiye anayesimamia mali yake wanadaiwa kuficha mamilioni ya pesa katika visiwa visivyotoza kodi vya Belize na Uruguay. Mamlaka ya ushuru ya Uhispania inadai walitumia visiwa hivyo kuficha malipo ya haki miliki ya sura ya mshambuliaji huyo.

Aidha wawili hao wanadaiwa kudanganya maafisa wa kukusanya kodi walipoulizwa awali katika uchunguzi huo. Upande wa mashtaka unataka wahukumiwe kifungo gerezani mbali na kutozwa faini kubwa ili iwe mfano kwa wengine wenye nia kama yao.

Chanzo BBC.