Katibu wa Chama cha mchezo wa Vishale TADA Kale Mgonja amesema, mashindano hayo yatashirikisha vilabu mbalimbali kutoka nchi hizo pamoja na wenyeji Tanzania.
Mgonja amesema, wanategemea kupata vilabu vingi zaidi kutoka katika nchi shiriki tofauti na mwaka jana ambapo vilabu kutoka nchini Kenya havikujitokeza kwa wingi.
Michuano hiyo ilifanyika mwaka jana mjini Dodoma ambapo nchi mwenyeji Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa jumla na katika mchezaji mmoja mmoja pia Tanzania iliweza kuibuka na ushindi huku Kenya ikiibuka na ushindi kwa upande wa wanawake na Uganda ikishika nafasi ya pili.