Kiungo mchezeshaji wa Manchester City Kelvin De Bruyne akiugulia maumivu baada ya kuumia kwenye mechi ya kombe la ligi dhidi ya Everton.
Hapo awali wakala wa kiungo huyo raia wa Ubeligiji Patrick De Koster aliarifu kuwa De Bruyne atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita lakini baada ya kukutana na daktari ikathibitishwa atakaa nje ya uwanja mwa wiki 10.
De Bruyne atakosa mechi 13 za mashindano mbalimbali msimu huu ikiwemo fainali ya kombe la ligi dhidi ya Liverpool Februari 28, mechi ya mtoano hatua ya 16 bora ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev na mechi dhidi ya mahasimu wao Manchester United ya Machi 20.
Kiungo huyo mchezeshaji ndiye mfungaji wa pili bora msimu huu nyuma ya Sergio Aguero akiwa amefunga mabao 12 kwenye mashindano yote barani Ulaya.

