
Kassim Mganga
''Akiongea kwenye Friday Night Live ya East Africa Television jana usiku, Kassim alifunguka juu ya mashabiki kumuita Mwinyi (yaani mtu anayevimba sana), kutokana na mtindo wake wa kutoa wimbo baada ya muda mrefu.
''Nadhani kupewa jina ni kitu cha kawaida kama halikutusi basi haina shida ila mimi naamini wananiita Mwinyi kwasababu natokea Tanga ambako Mamwinyi ni wengi'', alisema Kassim.
Mbali na hilo Kassim alifafanua kuwa hapendi kuchelewa kutoa wimbo lakini amejiwekea utaratibu huo kwasababu nyimbo zake zinahitaji uandishi wa ndani sana ndio maana sio rahisi kwake kutoa ngoma mara kwa mara.
Hata hivyo Kassim ameweka wazi kuwa kwasasa yeye na uongozi wake wa Manza Bay Music wameweka makazi ya kudumu jijini Dar es salaam, kwaaajili ya kuandaa kazi nyingi na baada ya ngoma mpya ya 'Silipizi' ambayo video yake aliitambulisha kwenye FNL zitafuata ngoma nyingi zaidi.