Kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Simba ikiwa katika picha ya pamoja katika moja ya mikutano mbele ya waandishi wa habari.
Kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya simba hii leo imepinga maamuzi ya shirikisho la soka nchini TFF kuitaka kamati hiyo kusimamisha mchakato wa uchaguzi na kusogeza mbele uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya simba Dr. Damas Ndumbaro amesema kuna sababu nyingi za kikanuni zinazowapa mamlaka wao kama kamati kuchukua maamuzi hayo.
Ndumbaro amesema moja ya sababu hizo ni kanuni ya uchaguzi ya TFF ibara ya 10 [6] toleo la mwaka 2013 inasema chombo pekee chenye mamlaka ya kufanya mabadiliko katika mchakato wa uchaguzi wa Simba ni kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo,
Kwa upande mwingine kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba imemwondoa katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais wa klabu ya simba mgombea aliyerejeshwa hivi karibuni Michael Wambura
Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr. Damas Ndumbaro amesema mgombea huyo pamoja na kuonywa kwa mara kadhaa na kwa maandishi lakini ameendelea kukaidi na kuvunja kanuni za uchaguzi wa klabu hiyo kipengele kinachokataza mgombea yeyote kuanza kampeni mapema kabla ya tarehe ama siku rasmi iliyotangazwa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo.