Katibu Mkuu wa Chama cha Judo nchini JATA Innocent Malya amesema, mashindano hayo yatasaidia kuweza kupata timu bora ya taifa ambayo itaiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Zanzibar hapo mwakani.
Wakati huohuo Malya amesema, mashindano ya kitaifa yaliyomalizika hivi karibuni yameweza kuwapatia vipaji vipya ambavyo vitaweza kuitangaza nchi katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.