Thursday , 4th Feb , 2016

Chama cha Judo nchini JATA kimesema kitatumia mashindano ya kanda ya tano ya Afrika Mashariki na kati kuweza kupata wachezaji watakaoweza kushiriki michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika Mwaka huu nchini Brazili.

Katibu Mkuu wa JATA Innocent malya amesema, kupitia mashindano hayo ambayo tanzania ndio Mabingwa watetezi watapata wachezaji wazuri ambao wataweza kupata timu nzuri itakayofanya vizuri nchini Brazili.

Malya amesema, mashindano ya Kanda ya tano yamepangwa kufanyika Februari 22 mpaka 29 mwaka huu nchini Burundi ambapo timu inaendela na mazoezi kwani wamejipanga kwa ajili ya kurudisha Ubingwa na kupata wachezaji watakaoshinda Medali za dhahabu kwa ajili ya ushiriki wao katika Olimpiki.

Malya amesema, wameweza kuwajenga wachezaji kisaikolojia pamoja na kuhamasisha vilabu kuwasimamia wachezaji katika mazoezi kwa ajili ya kuweza kushiriki mashindano hayo kwani muda umebaki mdogo sana ukilinganisha na maandalizi.