Saturday , 29th Apr , 2017

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba kindakindaki wameonekana kujawa na hofu katika kuelekekea mtanange wa Nusu Fainali za Kombe za Shirikisho FA dhidi ya Azam FC baada ya kusikia kurejea uwanjani kwa Nahodha John Bocco ‘Adebayor.

Kikosi cha Azam Fc kikiwa mazoezini

Katika siku za hivi karibuni mchezaji huyo alionekana kujumuika na wenzake mazoezi jambo ambalo limeonesha matumaini kwa timu ya Azam kupata ushindi katika mtanange huo endapo watapewa ruhusa ya kucheza kutoka katika benchi la ufundi la Azam.

Mchuano huo unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi huku historia zikiwa zinaonesha  kwamba itakuwa ni mara ya kwanza timu hizo mbili kukutana, ambapo ilirejeshwa msimu uliopita kufuatia kukosekana kwa misimu kadhaa.

Mshindi atayepatikana katika mechi ya kesho atakuwa amejikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika Fainali za Kombe la Shirikisho FA.

Pamoja na hayo, timu itakayoweza kushinda katika Fainali za mwisho itaweza kukabidhiwa zawadi ya Milioni 50 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo pamoja na kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika linalosimamiwa na CAF.