Kocha wa JKT Ruvu, Abdallah Kibaden
Kibeden amesema, wameshaanza maandalizi ya kujenga kikosi na anaendelea kuangalia kikosi cha vijana cha chini ya miaka 20 na watahakikisha wanasimama imara kupata wachezaji wazuri, wenye nidhamu ya hali ya juu na kuifikisha timu pale wanapopahitaji.
Kibaden amesema, katika zoezi zima la usajili hawagombanii wachezaji na wala wahategemei wachezaji walioachwa na vilabu vingine ndipo wawachukue kwani wanaangalia nidhamu na uwezo wa mchezaji kwani ndivyo vitaiweka timu katika nafasi wanayoihitaji wao.

