
Kikosi cha Serengeti Boys na Marekani kikiwa Uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India katika mchezo dhidi ya Marekani
Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime amesema, hali ya hewa kwa upande wao ni nzito kwani ni joto sana lakini haikuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo wa awali ningawa hawakuweza kushinda lakini walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Marekani.
Shime amesema, vijana wake wamejiandaa kwa ajili ya kupambana katika mchezo wa leo na hali ya hewa haitoweza kuwaathiri na wanaamini watarudi na faida mara baada ya kukamilika kwa michuano hiyo.
Shime amesema, mchezo wa awali umewajenga wachezaji wake na wanajua umuhimu wa mchezo wa leo na wanajiamini kuwa wanauwezo wa kucheza na timu yoyote.