
Cannavaro yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya kisigino.
Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, amesema wamemfanyia vipimo kwa mara ya pili beki huyo lakini inaonesha bado hajapona vizuri huku wakiwa hawajui lini ataweza kurejea uwanjani mpaka atakapoonana na daktari bingwa wa mifupa.
Matuzya amesema, baada ya kumfanyia tena vipimo, wamegundua bado hajapona vizuri, hivyo watamuweka bandeji ngumu (P.O.P) nyingine huku akiwa na programu ya kuonana tena na daktari bingwa wa mifupa kwa sababu alichoumia ni mfupa wa kisigino.
Matuzya amesema, Cannavaro ameumia muda mrefu na tatizo limekuja kuonekana baadaye sana na matibabu ya awali alipatiwa lakini mfupa haujaunga vizuri hivyo suala la kuwa sawa na kujiunga na timu inategemea na majibu ya daktari bingwa wa mifupa.