Friday , 2nd Jan , 2015

Mpambano usio wa ubingwa raundi 8 uzito wa kilo 70,uliowakutanisha mabondia Thomas Mashali na Abdalah Pazi ulivunjika baada ya kutokea fujo.

Mpambano huo uliopigwa usiku wa jana kwenye ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam uliishia raundi ya 3, baada ya kocha wa Abdallah Pazi, aliyejulikana kwa jina la Damme kwenda kambi ya Thomas Mashali kumpiga mtu na ndipo fujo zilipoibuka na mwamuzi kuvunja pambano.

Mwandaaji wa pambano hilo Doto Texas amesema Bondia Abdallah Pazi alifanya faulo kwa kumpiga kichwa Mashali na kumchana juu ya jicho, lakini mwamuzi hakusimamisha pambano.

Doto pia amesema mabondia wote wanatakiwa kukubali kurudiwa tena pambano hilo kwenye ukumbi wa PTA.