Thursday , 20th Nov , 2014

Timu ya Friends Rangers ya jijini Dar es salaam imesema ina uhakika wa kushiriki michuano ya ligi kuu msimu ujao kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya pamoja na nafasi waliyopo mpaka sasa.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu msaidizi wa timu hiyo, Hosea Abubakari amesema ligi ni ngumu lakini jinsi walivyojipanga pamoja na kuwa na kambi ya muda mrefu imewasaidia kwa ajili ya kuimarisha kikosi kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Abubakary amesema kila timu inahitaji kushika nafasi za juu zaidi ili kuweza kushiriki michuano ya ligi kuu lakini inategemea na mipango ikiwemo maandalizi ya timu ili iweze kufanya vizuri.