Wednesday , 15th Apr , 2015

Wapinzani wa Yanga SC katika Kombe la Shirikisho Afrika, Etoile du Sahel ya Tunisia wanatarajiwa kuwasili kesho (Alhamis April 16) tayari kwa mchezo wa Jumamosi utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Etoile itaongozana na ndugu zao Esperance ambayo inaelekea nchini Sudan kucheza na El Merreikh mechi za hatua ya awali ambapo Esperence itashushwa Sudan na safari ya Etoile itaendelea hadi Tanzania.

Mechi ya Yanga dhidi ya Etoile inatarajiwa kuanza saa tisa huku ikitarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka nchini Msumbiji ambao ni Samuel Chirindza ambaye atakuwa kati akisaidiwa na wasaidizi wake, Arsenio Chadreque Marengula na Celio de Jesus Mugabe.