Tuesday , 31st May , 2016

Timu za Clevaland Cavaliers na Golden State Warriors zitakutana kwa msimu wa pili mfululizo katika fainali ya ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA) itakayoanza kupigwa jumatatu ijayo.

Fainali hiyo inazikutanisha timu hizo baada ya kufanya vyema katika kanda zao, ambapo kwa Magharibi Golden State imeibuka kidedea baada ya alfajiri ya leo kuinyuka Oklahoma City Thunder, na huko Mashariki Cavalliers ikitamba mbele ya Toronto Raptors katika fainali ya ukanda huo.

Cavaliers ikiongozwa na Lebron James, itaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa katika fainali ya msimu uliopita mbele ya kikosi cha Warriors kilichokua moto wa kuotea mbali kikiongozwa na MVP, Stephen Curry.