Tuesday , 16th May , 2017

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF} limewateua watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi katika kusimamia mchezo wa Kundi A hapo kesho utakaowakutanisha Ghana na Gabon kwenye uwanja wa Port Gentil michuano ya Afcon U-17.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF}

Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine ambaye atakuwa Kamishna wa mchezo huo, Frank John Komba kupewa nafasi ya mwamuzi msaidizi pamoja na Dk. Paul Gaspel Marealle kushika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania  {TFF} imewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na CAF huku wakiwatakia kila la kheri atika kutimiza majukumu waliyopangiwa kesho na baadaye hasa ikizingatiwa kuwa fainali zijazo za vijana kama hizi, zitafanyika Tanzania mwaka 2019.