Tuesday , 16th Jun , 2015

Baraza la michezo nchini BMT limeitaka Shirikisho la Ngumi nchini BFT kuweka kambi au kutafuta mapambano ya ndani kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya All African Games inayoanza kutimua vumbi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzaville.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa BMT Henry Lihaya amesema, kama timu ya Taifa ya ngumi imeshindwa kwenda nchi yoyote kwa ajili ya maandalizi inauwezo wa kufanyia majaribio hapa nchini au kualika timu ambazo watafanya nao majaribio kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo.

Lihaya amesema hakuna fungu ambalo limetengwa kwa ajili ya timu hiyo kuwa na mapambano ya majaribio lakini kama itajibidiisha ikiwa ndani ya nchi wanaamini itaweza kufanya vizuri na kuipeperusha bendera ya nchi.