Thursday , 14th May , 2015

Mashindano ya Kick Boxing kwa ajili ya kumtafuta bingwa wa mabingwa katika mchezo huo yanatarajiwa kuanza rasmi Mei 17 jijini Dar es salaam kwa kuwa na mapambano mawili huku yakitanguliwa na mapambano mengine matano ya utangulizi.

Akizungumza na East Africa Radio, mratibu wa mapambano hayo Japhet Kaseba amesema wameamua kuirudisha ligi hiyo ambayo ilisimama miaka miwili iliyopita ili kuweza kupata bingwa ambaye ataweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya nje na ndani ya nchi.

Kaseba amesema katika pambano hilo la kutafuta Bingwa wa mabingwa litawakutanisha Chande Lee akipambana na Mrisho Dame huku Hamisi Mwakinyo akipambana na Ramadhani mshana huku.

Kaseba amesema, katika mapambano ya utangulizi yatawakutanisha Ibrahim Rajab akipambana na Swedy Kiumbe, Said Kasim akipambana na George Samwel, Frank Epimaki na Sadam Mapipi, Yusuph Habibu na Daud Gilbert huku Mwishehe Mwingila akipanda kupambana na Gulama Mapunda.