Sunday , 13th Nov , 2016

Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu ameamua kurejea kwenye timu hiyo baada ya ujio wa kocha mpya, George Lwandamina kutoka Zambia." 

Malimi Busungu

Busungu alikata tamaa kutokana na kutopewa nafasi ya kucheza chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm na akasusa tangu Oktoba 1, mwaka huu. 

Akizungumza jana, Busungu alisema alikuwa anaumia kuwekwa benchi Yanga wakati kwenye mazoezi alikuwa anafanya vizuri na makocha wanamsifia.
Busungu amesitisha uamuzi wake wa kuondoka Yanga baada ya mabadiliko ya benchi la Ufundi yanayotaka kufanywa na uongozi.

Yanga inataka kuondoa benchi zima la Ufundi Yanga, lililo chini ya Pluijm na wasaidizi wake.