Kikosi cha Azam FC
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi Dar es salaam Azam imejipatia mabao yake kupitia kwa mrundi Didier Kavumbagu dakika ya 9 ya mchezo, na bao la pili kupitia Nahodha wao John Bocco ‘Adebayor’ katika dakika ya 79 ikiwa ni dakika 2 tangu aingie kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche katika dakika ya 77 ya mchezo.
Katika mechi hiyo pia pamezuka malalamiko kutoka kwa mashabiki waliotaka kushuhudia pambano hilo na kuzuiwa kwa madai kuwa uwanja ulikuwa umejaa baada ya kufurika mashabiki na kufikia ukomo wa uwezo wake.
Mechi ya marudiano itapigwa wiki 2 zijazo nchini Sudani ambako Azam FC itatakiwa kutofungwa zaidi ya mabao 2-0 ili isonge mbele katika michuano hiyo ya kimataifa, ambayo kwa Azam hii ni mara yake ya Pili kushiriki tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007.
Kwa upande wao Yanga jana pia iliifunga BDF mabao 2-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.