Thursday , 7th Aug , 2014

Baada ya kupata nafasi ya kwenda kushiriki michuano ya kombe la Kagame nchini Rwanda, Uongozi Azam FC watamba kuonyesha makali yao na kurudi na ubingwa

Kikosi kamili cha azam fc ambacho hii leo kimekwea pipa kuelekea Kigali Rwanda.

Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 6 wa mabingwa wa soka Tanzania bara timu ya Azam FC wameondoka jioni ya leo kuelekea Kigali nchini Rwanda ambako watashiriki michuano ya klabu bingwa kwa nchi za Afrika mashariki na kati [kombe la Kagame ]

Azam FC imepata nafasi hiyo baada ya shirikisho la vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na kati CECAFA kuitosa Yanga kutokana na kutofuata kanuni za mashindano hayo

Ofisa habari wa Azam FC Jafar Idd Maganga [mbunifu] amesema wanataraji kuonesha makali yao katika mashindano hayo kwakuwa nafasi waliyoipata walikuwa wakiililia kwa muda mrefu na sasa wameipata

Aidha Jafar amesema awali walikuwa na lengo la kutafuta michezo mingi ya kimataifa ya kirafiki ili kujiweka sawa na ngarambe ya michuano ya ligi kuu pamoja na klabu bingwa ya Afrika lakini sasa wamepata bahati hii ambayo amekili kiukweli itawasaidia mno katika kutimiza malengo yao kwajinsi wanavyotegemea ushindani wa kutosha kutoka katika vilabu vitakavyoshiriki michuano hiyo msimu huu

Timu hiyo kesho inataraji kuanza kutupa karata yake ya kwanza ya kulisaka kombe hilo kwa kuvaana na timu ya Ryon Sports ya Rwanda mchezo utakaoanza saa 10 jioni.