Monday , 2nd Jan , 2017

Klabu ya Azam FC, imeanza vema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Zimamoto bao 1-0, mchezo uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mechi ya Azam na Zimamoto iliyopigwa leo

Winga wa kushoto wa Azam FC kutoka Ghana, Enock Atta Agyei, alianza kuichezea mechi ya kwanza ya mashindano timu hiyo tokea aliposajiliwa, ikiwa ni baada ya kushindwa kuitumikia kwenye Ligi Kuu kufuatia kutotimiza umri wa miaka 18, ambapo kwenye ligi ataanza kuonekana baada ya kutimiza umri huo Januari 5 mwaka huu.

Azam FC ilibidi isubiri hadi dakika ya 79 kuweza kuandika bao hilo la ushindi lililofungwa na mshambuliaji Shaaban Idd, aliyeitumia vema pasi ya juu ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Azam iko kundi moja la A na Yanga, Zimamoto pamoja na Jamhuri ya Zanzibar