
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii klabu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu imethibitisha kuwa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na mchezaji huyo raia wa Ghana na vilabu vingine visubiri muda mwingine.
Ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu hiyo umeandika, “Asante Kwasi akiwa chini ya himaya ya Singida United kabla hajaamua vinginevyo. May be NEXT TIME”.
Kwa upande mwingine kuna tetesi kuwa Mlinzi huyo tayari ameshasaini mkataba na vinara wa ligi Simba SC. Simba inadaiwa kumuacha nahodha wake Method Mwanjali na nafasi yake inatarajiwa kuzibwa na Asante Kwasi.
Shirikisho la soka nchini TFF lilifungua dirisha dogo la usajili Novemba 15 hadi Disemba 15, lakini kuna taarifa kuwa muda umeongezwa baada ya mtandao wa usajili wa shirkisho la soka la kimataifa FIFA kusumbua siku ya mwisho wa usajili.