Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, alipokuwa KIKAANGONi, leo
Akizungumza katika kipengele chaKIKAANGONI kinachorushwa LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, Bashe ameweka bayana kwamba kwa watu ambao walizoea kupiga dili kwa sasa hivi wamekwama mdiyo maana wanalalamika kuwa ni dikteta.
“Rais Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama maana halisi ya dikteta ilivyo , ila ni kiongozi ambaye ni mkali ambaye anapingana na mambo ya kufanya mambo kwa mazoeza 'Business as usual' waliokuwa wamezoea kupiga dili bandarini kwa siku mtu alikuwa anapata laki moja au mbili sasa hiyo imekoma” Amesema Bashe.
Aidha kuhusu baadhi ya wananchi kulalamika kwamba pesa hazionekani mtaani, Mbunge Bashe amesema kipindi alipoingia katika uongozi Rais Benjamin Mkapa wananchi walilalamika kwamba pesa zimepotea ila baada ya muda uchumi ukaimarika hivyo kwa sasa wananchi waipe muda serikali ya Rais Dkt John Magufuli.
Kuhusu jitihada za kuleta maendeleo Jimboni kake, Bashe ameeleza namna aambavyo ameanza kusaidia vijana ambapo baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kushona wamepelekwa Moshi kujifunza namna ya kutengeneza viatu vya ngozi kwa kuwa jimboni humo anatarajia kujenga kiwanda kidogo cha ngozi.
Pamoja na hayo Bashe amewataka wawekezaji ambao wanataka kwenda kuwekeza katika jimbo lake kwenda kwa kuwa watapatiwa ushirikiano wa kutosha na eneo la ardhi tayari lipo.