Monday , 10th Dec , 2018

Rapa Eric Msodoki a.k.a Youngkiller amemnyooshea mikono Big Chawa wa East Africa Radio, akidai ni mkali wa kuuliza maswali kwa viongozi wa serikali ndio maana ametumia kazi yake kwenye ngoma yake mpya.

Youngkiller Msodoki

Akiongea na Planetbongo ya East Africa Radio kuhusu uamzi wake wa kutumia 'video clip' ya mahojiano ya Big Chawa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juliana Shonza amesema ni kwasababu anakubali kazi ya Big Chawa.

''Napenda jinsi anavyofanya kazi zake na jinsi anavyouliza maswali yake haswa anapokutana na viongozi wa serikali'',  amefunguka Killer.

Katika wimbo huo mpya unaoitwa Sinaga Swaga Part 3, Youngkiller ametumia video ambayo Big Chawa alimuuliza Mh. Shonza juu ya nyimbo na wasanii anaowapenda ambapo waziri alimtaja Youngkiller.

''Nashukuru baada ya kumuuliza jibu lilikuja kuwa zuri kwa upande wangu kwahiyo ni kitu kikubwa ambacho isingekuwa vizuri kuacha kukitumia'', ameongeza rapa huyo kutoka Mwanza.