Friday , 5th Jun , 2015

Msanii wa kundi la muziki Yamoto Band, Aslay baada ya muda kupita akiwa katika mahusiano ya kimapenzi na msichana ambaye mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu ukaribu huo hatimaye atoa ya moyoni kuhusiana na mpenzi wake huyo.

msanii wa kundi la muziki la Yamoto Band Aslay akiwa na mpenzi wake

Aslay ameeleza kuwa hatua yake imetokana na kukumbwa na misukosuko iliyotokana na kufuatwa na wanawake wengi, kitendo ambacho kilipelekea kuwekwa chini na uongozi wake kuonywa na hatimaye kuamua kutulia na mpenzi wake aliyemtangaza.