Monday , 2nd Nov , 2015

Baada ya mwisho wa wiki kufanya shoo kali ya aina yake katika viwanja vya Leaders Club, nyota wa kimataifa Wizkid ambaye ni mara yake ya kwanza kutumbuiza Tanzania, ameeleza kuwa alikawiza ujio wake ili kufanya kazi na watu sahihi.

nyota wa muziki wa Nigeria Wizkid

Wizkid ambaye alikiri kuwa na mapenzi pekee na kuwakubali mashabiki kutoka hapa Tanzania, ameeleza kuwa amekuwa akiwasiliana na kupata maoni mbalimbali kwa njia ya mtandao, kumtaka kwa ajili ya kutumbuiza hapa nchini.

Kati ya mambo mengi aliyoongea pia, staa huyo akagusia chanzo cha wimbo wake mkali wa Ojuelegba alioufanya kubainisha msoto aliopitia kutoka maisha ya chini kabisa, ikiwa ni rekodi aliyoitengeneza kwa mitindo ya miondoko huru na kuirekodi mara moja pekee.

Wizkid pia akaeleza juu ya lebo yake kubwa ya Starboy ambayo inajihusisha na burudani kwa upana wake, akiwa amechukua wasanii wawili wapya atakaowatambulisha hivi karibuni.

Vilevile akamalizia kwa kueleza alichokuwa anakiwaza baada ya hatua yake ya kujaribu kumvuta msanii Dej Loaf kutoka Marekani katika himaya yake ya kimapenzi.

na hapa anaeleza mwenyewe juu ya ujio wake na kwanini wakati huu.