Tuesday , 17th Mar , 2015

Star wa muziki wa nchini Kenya, Willy Paul ameelezea furaha kubwa aliyonayo kwa njia ya mtandao baada ya kupata shavu kubwa la ubalozi wa bidhaa ya maji ya kunywa, ikiwa ni mkataba ambao umeweza kubadili kabisa maisha yake.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Willy Paul

Star huyo amesema kuwa, anamshukuru sana Mungu kutokana na kutokumbagua, akiwa ametokea katika maisha ya kawaida sana katika eneo la makazi duni la huko Mathare.

Sambamba na shavu hili, star huyo amesema pia kuwa anafurahi kuona rekodi zake mbili, Tam Tam na Mamangu zikiendelea kupata mashavu ya muda wa hewani katika vituo mbalimbali nje ya mipaka ya Kenya, katika kudhihirisha kuwa sanaa yake kwa sasa imepiga hatua kubwa mbele.