Friday , 28th Mar , 2014

Kundi la WEUSI rapa Joh Makini, G Nako pamoja na Nikki Wa Pili ambao wamekuwa huko Nairobi nchini Kenya kwa siku kadhaa sasa, wameweza kufanya mchongo wa kutengeneza video ya ngoma yao ya Gere ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali kwa sasa.

Video ya ngoma hii ni kazi nyingine kubwa ambayo inatarajiwa kutikisa ulimwengu wa burudani pindi itakapotoka.

Katika ziara yao hii huko nchini Kenya, Wasanii hawa wanaoiwakilisha poa Bongo, wameweza kukutana na mastaa wa muziki Afrika Mashariki, Akiwepo Navio wa nchini Uganda, Kundi la P Unit, Nazizi, Collo pamoja na wengine ambapo tayari mipango ya kolabo kati yao imekwishawekwa sawa.

Wasanii hawa pia wameweza kutumia muda huu kutengeneza Remix ya ngoma yao ya Gere ambayo itakuwa na mastaa wakubwa kabisa wa nchini Kenya.

WEUSI pia wamepata nafasi ya kufanya kazi kwa karibu na producer Sappy huko Nairobi, kati ya michongo mingine, na kuifanya ziara yao hii kuwa ya mafanikio na matarajio makubwa.