Msanii wa kundi la Goodlyf nchini Uganda Weasle akiwa na mpenzi wake Samira.
Weasle ameelezea kuwa amefarajika baada ya kumtambulisha katika familia ya Samira huku ikielezwa kuwa Samira ameweka nia ya kuwaona watoto wake Weasle alipokuwa katika mahusiano yake ya awali.
Weasle alielezea mwenyewe kuwa baada ya mahusiano na mwanamitindo Carol mwenye makazi yake nchini Sweden, kwa sasa ameamua kutulia na Samira huku wakiwa na mipango mingi katika mahusiano yao.