
Jaji wa Shindano la Dance100 Lotus akionyesha alama kwa moja ya kundi lililoshiriki usaili viwanja vya Don Bosco Upanga Dar es salaam.
Akizungumza na EATV mara baada ya shindano hilo mmoja wa majaji wake Lotus amesema jambo ambalo ameligundua kutoka kwa washiriki ni kutozingatia muda wa dakika tano katika kupangilia waanze na nini na wamalizie na jambo gani ambalo linaweza kupelekea kutoa alama nzuri zaidi.
''Muda ni jambo muhimu sana kwenye usaili wa jukwaani kwa kuwa tunapoona kundi linaingia tunaangalia mbwembwe zisizidi dakika mbili ili dakika nyingine zitumike kwenye kucheza kwa kuwa shindano ni la kucheza na siyo manjonjo pekee'' Amesema Jaji Lotus.
Jaji huyo amewataka washiriki ambao wanatarajia kujitokeza katika usaili wa mwisho katika viwanja vya TCC Chang'ombe siku ya Jumamosi tarehe 30.07.2016 kuhakikisha wanajipanga vyema kwani usaili ni mgumu na makundi ni mengi ambayo yanatarajia kuonyesha uwezo wao katika jukwani