Sunday , 13th Sep , 2015

Bendi kongwe ya muziki wa miondoko ya mduara nchini The Kilimanjaro Music Band 'wana Njenje' wanatarajia kuingia studio kurekodi wimbo maalum kwa ajili ya mwimbaji wao Bwana Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama 'Babu Njenje' ambaye ni mgonjwa.

Bendi kongwe ya muziki wa miondoko ya mduara nchini The Kilimanjaro Music Band 'wana Njenje'

Mwimbaji wa bendi hiyo maarufu nchini Waziri Ally ameiambia enewz kuwa ni muda mrefu walikuwa wanamsubiria mwanamuziki huyo afya yake iimarike baada ya kupatwa na stroke ya muda wa takribani miaka miwili iliyopita.

Waziri amesema kuwa hivi sasa hali ya Babu Njenje inaendelea vizuri na wameona ni wakati muafaka wa kuingia studio ili kurekodi albamu yao mpya ambayo inatarajiwa kutoka ndani ya mwaka huu.