Wasanii waliofanikiwa kupenya kwenye EATV Awards wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa kwa ajili yao.
Wakizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, wasanii hao wamesema tuzo zitaleta changamoto kwao na kwa wasanii wengine, hivyo kilichobaki ni kwa mashabiki kurudisha fadhila kwenye kazi zao, kwa kuwapigia kura ili waweze kutwaa tuzo hizo na kwenda nazo nyumbani.
G Nako ..." Mtu anapofanya kitu kizuri ni wajibu kwa wananchi kurudisha heshima kwake, hivyo ni wakati wa mashabiki kutupa ushindi, pia zimekuja kama chachu ya watu wengine, makampuni na media nyingine, waone wajibu wa kuanzisha kwa sababu zinakuza muziki wetu, ni kitu kizuri lakini pia ni ushawishi kwa wengine".
Shetta........."EATVAwards imenipa pumzi na kunijulisha kuwa ukiwekeza inalipa, yani imenifuta machozi, hii ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye tuzo mimi kama mimi zaidi ya ambayo niliwahi kuingia kama collabo, mi niko happy, hayo mengine i don't care".
Ben Pol........."Palipo na wengi hapaharibiki neno, mi nimefurahi kufanikiwa kuingia, hii imeonesha ni kiasi gani kazi ninazofanya zinakubalika kwa jamii, lakini pia ni changamoto kubwa kwenye game yangu".
Sherehe za utoaji tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 10 Desemba 2016, na ukitaka kujua jinsi ya kumipigia kura msanii unayempenda ingia www.eatv.tv/awards