Wednesday , 13th Jul , 2016

Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma Jaji mstaafu Salome Kaganda amewataka wakurugenzi 185 walioteuliwa kuiheshimu kazi yao na kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za sheria za umma.

Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma Jaji mstaafu Salome Kaganda

Jaji Kaganda ameyasema hayo alipokuwa akiwaapisha wakurugenzi ambao waliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

''Mkajiheshimu, mjue kwamba kuna jambo moja unaweza kufanya likakudhalilisha wewe pamoja na familia yako na ukoo wako kwa ujumla kama wewe ni mwanamke ujue cheo ulicho nacho ni dhamana kwako na siyo kwa mumeo, kuna watu unakuta hadi wenza wao wanataka kuamrisha magari ya serikali yatumike kwa ajili yao, cheo umeaminiwa wewe na siyo mwenza wako'' amesema Jaji Kaganda.

''Enendeni mkafanye kazi na mjitambue kwamba madaraka yanaleweshya , na ninyi wengi ni vijana hivyo kuweni makini sana , wazee wamewapisha ninyi ili mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu''amesema Jaji Kaganda

''Sasa msipokuwa makini hata kwa mavazi na mwonekano tuu mtadharauliwa, mfano utasikia binti anasema yule mkurugenzi wa Halmashauri ile hamna kitu anakoroma sana usiku, sasa tutajiuliza alikusikia wapi?'' Amesisitiza Jaji Kaganda.

Wakurugenzi walioteuliwa wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vyema mapato ya serikali ikiwa ni pamoja na kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa