Wednesday , 4th Mar , 2015

Rapa Wakazi amewataka vijana kufahamu kuwa nguvu waliyonayo kuamua mustakabali wa nchi kutokana na wingi wao, na kufahamu kuwa maisha yao ya baadae yatatafsiriwa kutokana na maamuzi ambayo wanayafanya sasa.

msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Wakazi

Wakazi ametoa kauli hii kuunga mkono kampeni ya ZamuYako2015 inayoendeshwa na EATV na East Africa Radio, na kuongeza kuwa, vijana wanatakiwa kuichukulia kampeni hii kwa uzito wake na si kama kampeni ya kawaida.