Tuesday , 30th Jun , 2015

Rapa Wakazi amesema kuwa, familia yake imekuwa na mchango mkubwa kama dira kwa maisha yake ya binafsi na ya kimuziki, tofauti na watu wengine ambao hutazama wale waliofanikiwa zaidi katika fani ambazo wanajihusisha nazo.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Tanzania Wakazi

Wakazi pia amewapa shavu ndugu zake Ester Wassira na Lady Jay Dee kama watu ambao anajifunza mengi kwao kimuziki, kaka zake, wazazi na pia wadogo zake ambao wanamjenga kila siku katika nyanja mbalimbali.