Monday , 6th Oct , 2014

Rapa wa muziki, Wakazi, amezungumzia swala la kazi nyingi nzuri za Hip Hop kukosa video na pia kuchukua muda mrefu katika matayarisho yake na kusema kuwa, wasanii hao wanajitahidi sana ila tatizo linakuja katika gharama kubwa za kazi hizo.

msanii wa hip hop nchini Tanzania Wakazi

Wakazi amesema kuwa, wasanii hawa wanajitahidi sana, akitolea mfano wa kazi zake nyingi kuwa na video, na kusisitiza kuwa, swala la uwezo kiuchumi mara nyingi linakuwa ndio kikwazo cha jitihada za wasanii hawo.