Monday , 20th Apr , 2015

Akiwa kama moja ya wasanii wanaounga mkono kampeni ya Zamu Yako 2015, mbali na kuwataka vijana kujihusisha katika uchaguzi mwaka huu, rapa Wakazi ametaka kundi hilo pia kufuatilia na kuwafahamu vizuri wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali.

msanii wa muziki wa bongofleva Wakazi

Wakazi amesema hayo kuwafungua macho vijana ili uchaguzi wao uende sambamba na matokeo katika suala zima la utendaji kazi wa viongozi hawo, vilevile akiwataka vijana hao kujihusisha pia katika kuwania nafasi za uongozi ili kuleta mabadiliko.