Wednesday , 8th Jul , 2015

Baada ya ukimya mrefu diva nyota wa nchini Kenya Wahu Kagwi ambaye amekuwa bize katika malezi ya watoto na kazi zake binafsi tayari ameamua kuchokoza mashabiki kwa kuposti picha akiwa studio na nyota wa muziki wa gospel nchini.

Mkali huyo wa kibao kikali cha 'Sweet Love' akiwa studio na mwanae ameposti picha akiwa sambamba na wasanii nyota wa miondoko ya gospel wakiwemo Size 8 na Bahati na mkali wa michano Collo akionesha kuwa muda na wakati wowote mambo mazuri yanakuja.

Wahu aliandika katika mtandao akimwagia sifa rapa Collo kwa kazi yake nzuri ya utunzi wa nyimbo na pia kuwapa sifa wakali wa nyimbo za gospel Size 8 na Bahati.