Saturday , 22nd Aug , 2015

Video Queen wa Kibongo na Msanii wa filamu kutoka nchini Tanzania Rechel Njingo amechaguliwa kushiriki katika tuzo za Nyambago Awards kama Best Actress kutoka Central Zone kupitia movies yake ya Clarita ambayo inafanya vizuri kwa sasa.

RECHO

Tuzo hizo ambazo zinashirikisha mikoa yote ya katikati mwa Tanzania ndiyo tuzo za pekee zinazowatambua wasanii kutoka katika mikoa hiyo ambao wanakuwa wamefanya kazi zinazoitambulisha tasnia ya sanaa nchini.

Katika kuonesha kuwa kuchagulia katika tuzo hizo ni halali ya yake video qeen huyo aliyefanya kwenye nyimbo mpya ya PNC amesema kwa sasa yuko location wakiandaa movies nyingine huku akiwataka wadau wa filamu nchini kuwapa sapoti ya kutosha katika kufanikisha kusonga mbele zaidi.