Wednesday , 4th Jun , 2014

Mchekeshaji maarufu wa nchini Kenya Vincent Muasya a.k.a Chipukeezy Vinie anayekubalika kutokana na fani yake hiyo kimataifa amekula shavu la kutumbuiza Jijini London nchini Uingereza, Nigeria na Afrika Kusini.

Vincent Muasya aka Chipukeezy Vinie

Vincent anatarajia pia kutumbuiza kwa mara ya pili katika tamasha maarufu la uchekeshaji barani Afrika liitwalo Nite of a Thousand Laughs, linalowaunganisha nyota mbalimbali katika fani hiyo.

Chipukeezy Vinie kama ambavyo hujulikana kwa jina lake la kisanii ameelezea furaha yake ya kuweza kutimiza ndoto zake kwani ziara hizo kubwa zinatarajiwa kuanza ndani ya miezi miwili ijayo.