Friday , 16th May , 2014

Baada ya kungojewa kwa muda sasa, Video ya mwanadada Mwasiti ya ngoma yake ya Serebuka, hatimaye inatarajiwa kuzinduliwa leo na kuonekana kwa mara ya kwanza kabisa kupita show kali Afrika Mashariki ya Friday Night Live usiku wa leo kupitia EATV pekee

Mwasiti

Kazi hii safi ya muongozaji video Nick Dizzo, ni moja ya kazi ambazo Mwasiti akiwa na sapoti kubwa ya wasanii wenzake amesema kuwa imefanyika kwa ushirikiano mzuri sana na timu yote iliyoshiriki, na pia baada ya kukamilika, ikapatiwa muda wa kutosha kuifanyia marekebisho na maboresho kabla ya kuwa tayari kwa kuwafikia mashabiki.

eNewz inakupatia nafasi hapa ya kutazama kipande hiki cha video leo saa mbili kasoro dakika tano usiku, na usikose Friday Night Live leo kuanzia saa nne usiku kwa 'official premier' ya kazi hii ambapo atakuwepo Mwasiti mwenyewe kuitambulisha.