Saturday , 2nd May , 2015

Staa wa muziki Cyrill Kamikaze, siku nne tu baada ya kutoka kwa video ya ngoma yake ya Nikikuona aliyoifanyia nchini Kenya, ameanza kujivunia mafanikio ya kazi hiyo, ikiwepo kuinyanyua rekodi ya ngoma hiyo ambayo ilitoka takriban miezi 2 iliyopita.

Cyrill Kamikaze

Hii ikiwa ni moja ya project kubwa kabisa kwa Cyrill kuwahi kufanya, nyota huyo wa muziki amesema kuwa ameendelea kupata feedback nzuri kutoka sehemu mbalimbali, dalili nzuri inayodhihirisha kazi kubwa aliyoifanya pamoja na director. wa kazi hiyo, Young Wallace.

Kupitia video mpya ya Nikikuona, ubora wa picha na vilevile mpangilio wa kisa ndani ya video hiyo, msanii huyo ametengeneza muendelezo wa kuendelea kunguruma katika chati za vituo mbalimbali ndani na nje ya Afrika Mashariki.