Ben Pol pamoja na Patricial Hillary
Ben Pol pamoja na Patricial Hillary, wamewataka wapenzi na mashabiki kutokosa onesho hilo kutokana na vile walivyojipanga kiburudani.
Katika onesho hilo lililodhaminiwa na East Africa Radio na East Africa Television, wamejipanga kufanya burudani ya live iliyotulia na yenye urefu wa kutosha, huku Patricia akiahidi kukumbushia ladha za zamani na maneno yao yakienda sambamba na vionjo vya kile walichopanga kufanya.
Usikose kuhudhuria onesho hilo la kudhihirisha upendo wa dhati katika Siku ya Wapendanao kwa kiingilio cha shilingi 70,000 tu kwa mtu mmoja, na 120,000 kwa watu wawili.





.jpg?itok=5cvL0YaP)