Raymond akiwa kwenye kipindi cha FNL, EATV
Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Raymond alisema yeye kama msanii mchanga kwanza amezifurahia tuzo hizo kwani zina mchango mkubwa sana, ikiwemo kuongeza juhudi zaidi ili aweze kuishinda na kujiwekea misingi mizuri.
“Nilifurahi kwa sababu inakuwa inaonesha picha nzima ya muziki jinsi unavyokwenda, mtu akiona jamaa kachukua tuzo na mimi nifanye juhudi na mimi nichukue, nimefurahi sana uwepo wa tuzo ni kitu kizuri kinaonesha thamani ya muziki wetu”, alisema Raymond.
Tuzo hizo ambazo zitafikia kilele chake tar Desemba 10, 2016, zinahusisha wasanii wa filamu na muziki kwa nchi za Afrika Mashariki, na pia ndizo tuzo kubwa za kwanza kuanzishwa Afrika Mashariki na kushirikisha wasanii wake moja kwa moja.