T.I.D MNYAMA
Baada ya kutusubirisha kwa muda mrefu hatimaye TID azindua video yake ya Confidence usiku wa Eid na kufanya show moja kali wakisimama watu wawili tu TID Mzee kigogo na KR Mulla.
Lakini kubwa sasa ni kwamba chupa limezinduliwa lakini hautaliona kwenye TV yako kwa sababu TID mwenyewe ametoa maboko ya kutosha ndani ya hiyo video kiasi anajishtukia kutoa video hiyo na kuamua kutaka kuirudia.
Hata hivyo T.I.D amewaambia wapenzi wake kuwa msafiri alifanya kazi yake vizuri lakini kwa upande wake kuna baadhi ya vitu ambavyo imeonekana kukosekana katika video hiyo hivyo kuna baadhi ya vitu vitaongezewa.







